Timu ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ikisaini Mkataba na Kampuni ya M/S Siangxi Geo Engeneering(Group) Corportion kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu mbalimbali
Mradi wa Uendelezaji Miji Mkakati (TSCP) umeendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani baada ya jana kusaini mkataba wenye gharama ya shilingi bilioni 21,676,274.58 na kampuni ya M/S Siangxi Geo Engeneering(Group) Corportion kutoka China kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali.
Ujenzi wa miundombinu hiyo utasaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ujaaji wa maji ya mvua zinazosababisha athari kwa jamiii kiwa ni pamoja na vifo na uharibifu wa mali za wananchi, ukosefu wa sehemu za kupumzikia, uwepo wa soko dogo ambalo halikidhi mahitaji.
Akizungumza kwenye sherehe za kusaini Mkataba huo zilizofanyika Juni 8,2018 kwenye Ofisi ya Mstahiki Meya, Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi Betarice Dominic ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuleta miradi kwenye Manispaa inayoenda kutatua chagamoto nyingi na kuitaka kampuni hiyo kufanya kazi kwa weledi kama mkataba unavyiotaka ili kazi ikamilike kwa wakati.
Aidha amesema kuwa manispaa inafanya shughuli nyingi za kusaidia jamii kwa kushirikiana na wadau hivyo ana amini ujio wa kampuni hiyo watashirikiana pamoja katika kusaidia jamii ya Manispaa
“kwa sasa sisi na ninyi ni marafiki ni imani yangu kuwa tutafanya kazi pamoja na kwa kushirikiana ikiwemo kusaidia jamii inayotuzunguka kwenye mambo mbalimbali yanayowahusu ikiwemo afya elimu” . Alisema Beatrice.
Mhe. Geofrey Mwanichisye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani amesema kuwa nchi ya China na Tanzania zina historia kubwa hivyo anaamini Kampuni hiyo itafanya kazi kubwa na nzuri na kuwataka kukamilisha kazi hizo kwa wakati kama ilivyopangwa.
Nae Meneja Mradi wa kampuni hiyo Chen Xianghua ameahidi kufanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa na kuwa ana imani kazi hiyo itakamilika kwa wakati kama mkataba unavyosema.
Kwa upande wake Isaac Mpaki mhandisi wa Manispaa amesema kuwa mkataba huo utatekelezwa kwa muda wa miezi 15 na kutaja miradi itakayojengwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa stendi ndogo ya mabasi Mikindani, Ujenzi wa soko Chuno,Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami (COTC,Shangani-Chuno na Senegal), Ujenzi wa mfereji wa kuondoa maji ya Mvua kutoka Skoya-Nabwada,Sido,Shakuru ,maghalani kuelekea bonde la Mtepwezi.hadi baharini, uboreshaji wa sehemu za kupumzikia Mashujaa, Tilla na Maduka Makubwa.
Manispaa imeanza kutekeleza Mradi wa Uendelezaji Miji Mkakakati tangu mwaka 2010 ukijenga miradi ya barabara(bandari, Zambia, Kunambi, Chuno na Mikindani), Ujenzi wa dampo kuu la Kisasa Mangamba pamoja na ujenzi wa vizimba 25 vya kuzolea taka,Ununuzi wa magari ya kuzolea taka na Mitambo,Ujenzi wa maabara ya kupimia udongo,ununuzi wa magari sita ya Ofisi. Aidha fedha zote zinazotumika kujenga miundombinu hiyo zinatoka Benki ya Dunia Ukiwa kama Mkopo kwa Serikali na kusimamia na Ofis ya Rais-TAMISEMI
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.