Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Juliana Manyama amewataka Wakuu wa shule za Sekondari zilizopokea fedha za ujenzi wa madarasa kuhakikisha wanafuata taratibu za manunuzi na kuzingatia ubora wa vifaa vya ujenzi vinavyonunuliwa ili kujenga madarsa yaliyo imara.
Manyama pia amewasisitiza Wakuu hao wa Shule kuhakikisha wanazishirikisha kamati za ujenzi za shule pamoja na kuwahimiza wajumbe wa kamati hizo kutimiza majukumu yao kwenye kila hatua ya ujenzi inapofanyika.
Aidha amewataka kuwa makini kwenye utunzaji wa nyaraka zote za ujenzi na kuhakikisha wanafungua “file” maalumu kwa ajili ya kutunza nyaraka hizo.
Manyama ameyasema hayo leo Oktoba 25, 2022 alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa ishirini na moja ya Sekondari yanayojengwa kwa fedha zilizotolewa na Serikali Kuu shilingi milioni ishirini (420,000,000) ikiwa ni maandalizi ya kujiunga na kidato cha kwanza 2023.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.