Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu. Ismail Ali Ussi ameridhia kuweka jiwe la Msingi jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD) lililojengwa katika Zahanati Mtawanya na Manispaa ya Mtwara Mikindani kwa fedha za mapato ya ndani shilingi milioni mia moja arobini na tatu mia nne hamsini na tisa (143,459,000) ili Kuboresha, kurahisisha na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.
Ndugu amesema kuwa Mwnge wa Uhuru umejipnea mradi mkubwa ambao unaenda kutatua maattqizo ya wananchi wa Kata ya Mtawanya
“Tumeenda kukagua mradi kwa kweli kimezingatia mahitaji yote ya wananchi, nimefurahi kuona katika jengo hilo kuna huduma ya kujifungulia, hongerereni uongozi wote” amesema Ndugu Ussi
Aidha amewaomba wananchi kuhakikisha wanaoitunza na kulinda majengo yote ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.
Kwa uapnde wake Mstahiki Meya Mhe. Shadida Ndile amesema kuwa Manispaa imeendelea kutekeleza maagizo ya Serikali na kwamba Manispaa imetoa fedha za Mapato ya ndani kujenga jengo hilo.
Awali akisoma taarifa ya mradi huo, Mganga Mfawidhi wa Kituo hiko Dkt. moses Julius Chayeka amesema kuwa Zahanati hiyo inahudumia wakazi wa Kata ya Mtawanya 7183 pamoja na wananchi wa maenep ya jirani na kwamba uwepo jengo hilo utawezesha kutoa huduma bora kwa jamii pamoja na kuwapunguzia adha wananchi ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Aidha ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma za afya hapa nchini.
Ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje zahanati ya Mtawanya
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.