Mbawala Chini Wahamasishwa Ujenzi Wa Zahanati
Wananchi wa Mtaa wa Mbawala chini Manispaa Mtwara-Mikindani wametakiwa kuendelea kujitolea kwa hali na mali katika kufanikisha ujenzi wa Zahanati katika Mtaa wao.
Ujenzi wa Zahanati hiyo utasaidia kuondoa adha inayopata Wananchi wanapougua kwa kuwa umbali uliopo kutoka mbawala chini hadi ilipo zahanati kwa sasa ni km 15 .
Akizungumza katika mkutano wa Uhamasishaji uliofanyika julai 19 Mbawala chini ,Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda alisema kuwa pamoja na Wananchi hao kutambua kuwa suala la Maendeleo linawagusa na kuamua kutoa eneo hekari 5 na matofali 4000 kwa ajili ya ujenzi huo, bado Wananchi wanatakiwa kuendelea kujitolea hadi Zahanati hiyo itakapo kamilika.
Aidha Mmanda alisema kuwa pamoja na wao kuonesha juhudi hizo Ofisi ya Mkurugenzi ya imewaunga mkono na imetenga kiasi cha Tsh milioni 40 katika bajeti yake ya 2017/2018 kwa ajili ya ujenzi huo, na Milioni 20 iko tayari na itatolewa karibuni.
Pamoja na hayo Mmanda amewataka Wananchi hao kuchangia na kujiunga kwenye mfuko wa bima ya afya (TIKA) ambayo inagharimu kiasi cha Shs 5000 kwa kila mmoja kwa mwaka mzima kwa kuwa ugonjwa haupigi hodi.
‘’Tunaweza kujenga hospitali hapa siku ugonjwa ukikukuta huna pesa mfukoni na haujakata bima ya afya ni sawa na kazi bure hospital haitakusaidia kitu ninawaomba mkakate bima ya afya’’alisema Mmanda.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara- Mikindani Beatrice Dominic amesema kuwa ana imani kuwa Wananchi watakuwa tayari kuchangia na kwamba hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa fedha baadhi ya majengo yatakuwa yameshakamilika.
“Nitafurahi sana kama wananchi wa mbawala chini tutakuwa tayari kuchangia tukitoka hapa na kwamba hadi kufikia mwisho wa mwaka 2017/2018 vyumba vichache vya zahanati vitakuwa vimeshakamilika”alisema Beatrice.
Awali akisoma taarifa ya Mtaa huo Kaimu Afisa mtendaji wa Kata Hamisi adam alisema kuwa pamoja na Wananchi kutoa hekari 5 na tofali kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati bado Mtaa unakabiliwa na tatizo la kutokuwepo kwa maji safi na salama, barabara mbovu kutoka Mbawala chini hadi Naliendele pamoja na kutokwepo kwa Zahanati.
Nae MHE Diwani wa Kata ya Naliendele aliwashukuru viongozikwa kukubali kufika Mwawala chini kwna kujionea wao wnyewe hali halisi iliyopo na kuahidi yeye na Wananchi kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha ujenzi wa zahanti hiyo inakamilika.
‘
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.