Kikundi cha wanawake wa Miseti (Miseti Women Group) kinachojishughulisha na utunzaji wa mazingira ya bahari kwenye upandaji wa mikoko katika Kata ya Chuno iliyopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani kimekabidhiwa vifaa vya usafi na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga Leo Oktoba 2, 2024 katika Ofisi za Kata hiyo.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mhe. Mtenga amekipongeza kikundi cha Miseti kwa kazi kubwa wanayoifanya na amewaahidi kuwa nao bega kwa bega katika kuhakikisha kuwa mazingira ya bahari yanakuwa safi na salama wakati wote ili kutunza viumbe vilivyopo baharini.
Aidha kuelekea zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Mhe Mtenga amewahamasisha akina mama hao kujitokeza kwenye zoezi la uandikishaji litakaloanza Oktoba 11 hadi oktoba 20 mwaka huu ili waweze kupiga kura na kuchagua kiongozi atakayewaletea maendeleo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Chuno Mhe. Fanikio Chijinga amempongeza Mbunge huyo kwa kuyasikiliza maombi ya wanakikundi na kuwapatia vifaa vitakavyosaidia kurahisha utendaji wao wa kazi za kila siku.
Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi wenzake, Bi Mwanampya Haji ,Mwenyekiti wa kikundi hiko amemshukuru Mtenga kwa kuwakabidhi vifaa hivyo na wameahidi kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na "gumboot"seti 11, Fagio za miti 15, reki 5, Chep
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.