Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga Julai 28,2021 amekabidhi mabati 160 katika shule za msingi tatu zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Mhe. Mbunge amekabidhi mabati hayo ikiwa ni muendelezo wa ari ya kuunga mkono juhudi za ujenzi na ukarabati unaoendelea wa miundombinu mbalimbali katika shule za Msingi.
Amezitaja Shule zilizopata mabati ni pamoja na Shule ya Msingi Kambarage mabati 60, Likombe 50 na Mitengo mabati 50.
Pamoja na makabidhiano hayo Mhe. Mtenga amewataka wazazi kushirikiana na walimu katika kudhibiti utoro wa wanafaunzi ili kuongeza ufaulu na kuimarisha sekta ya Elimu.
“Kudhiti utoro sio suala la walinu peke yao hawaliwezi, ndio tunapofeli wazazi tunadhani kuwa mtoto anapokwenda shule tumemaliza majukumu yetu, hii sio kweli niwaombe ndugu zangu tushirikiane na walimu ili tuweze kuondoa changamoto hii” Amesema Mhe. Mtenga.
Ameendelea kusisitiza kuwa njia mojawapo ya kuondokana na changamoto ya utoro ni wazazi kuhakikisha wanafuatilia taarifa za maendeleo ya mwanafunzi na kutoa taarifa kwa walimu wapoona mabadiliko hasi ya wanafunzi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.