MBUNGE VITI MAALUMU AGAWA TRUCKSUIT 100 KWA KIKUNDI CHA MICHEZO CHA AKINA MAMA
Mbunge Viti Maalumu Mhe Annastanzia Wambura amegawa nguo za mazoezi (trucsuiti) 100 zenye thamani ya shilingi 2,600,000 kwa klabu ya mazoezi ya akina mama wa Kata ya Tandika na Chikongola.
Trucksuit hizo zenye thamani ya shilingi milioni 2,666,000 zimetolewa na Mfuko wa hifadhi ya Jamii (PPF) kupitia mbunge huyo ikiwa ni kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais liilotaka Wananchi kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao
Akizungumza katika tukio la ugawaji wa nguo lilifanyika disemba 16 mwaka huu kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Majengo Wambura amewapongeza akina mama hao kwa kuweza kujikusanya na kuanzisha kalbu hiyo ya mazoezi kwa kuwa mazoezi yanasaidia kuimarisha mwili na yanaimarisha mahusiano baina yao.
Amesema kuwa amefurahi kuona kikundi hiko kimeongeza wanachama wapya wakiwemo watoto kwani imekuwa ni fursa nzuri kwa wazazi kuzungumz nao kuhusu maadili na kuwataka kila baada ya muda wa mazoezi kuisha wazungumze nao, Aidha amesema uwepo wa watoto hao kwenye mazoezi utawasaidia kujiepusha na mambo mbalimbali ya Anasa.
Pamoja na hayo Wambura amewataka wana kikundi hao kujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiriamali kwa kuwa anaamimi kuwa kama wameweza kujitoa kufanya mazoezi basi hawashindiw kufanya shughuli za ujasiriamali ambazo zitawapatia kipato cha ziada.
Aidha Wambura alimpongeza Mkurugenzi wa Manispaa kwa kuwaunga mkono wanawake ikiwemo utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali na kumuomba awasaidie akina mama hao ili waweze kupata mikopo lakini pia kusawazisha kiwanja wanachofanyia mazoezi.
Kwa upande wake Katibu wa kikundi hiko Fatuma Jana amesema kuwa kikundi kimeshachagua uongozi na wameshaanza kuchangishana fedha shilingi 1000 kila Jumamosi na kwamba hadi sasa wana fedha taslimu shilingi 250,000 na wako mbioni kujisajili .
Amesema kuwa kama kikundi wamekubaliana wafanye kazi za pamoja ingawa kila mmoja ana shughuli zake binafsi hivyo wameamua wafanye shughuli za kilimo na kwamba wanaomba wapatiwe eneo la kilimo ili waweze kulima kwa pamoja
Aidha amewashukuru PPF kwa msaada wa kuwapatia nguo hizo na kwamba idadi ya wananchama imeongezeka hivyo wanaomba wasaidiwe tena ,Pia amewakaribisha wananchi wengine waende kujiunga kweye mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa amewapongeza wanakikundi hao kwani wanachokifanya ndo uchumi wenyewe kwa kuwa wasipofanya mzazoezi afya inaweza ikaterereka na wakashindwa kufanya shughuli za ujasiriamali.
Mkurugenzi Amesema kuwa Manispaa imeendelea kutii agizo la Serikali la kutenga asilimia kumi kwa ajili ya Mfuko wa Wananwake na Vijana na kwamba hivi karibuni manispaa imetoa shilingi milioni154.1 kama mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana na kwamba fedha zingine zimebaki kwenye mfuko.
Amewasisitiza akina mama hao kubuni njia nzuri za kufanya biashara zao ziwe zenye ubora na kwamba wanaposikia viwanda vidogo sio mpaka uwe na mashine kubwa kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa. Aidha amewaahidi akina mama hao kabla ya kujisajili atawapatia wataalamu wa Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kuwapa mafunzo yatakayowawezesha kufanya ujasiriamali wao vizuri.
Aidha amesema kuhusu changamoto ya eneo kwa ajili ya wajasiriamali ameahidi kukutana na diwani ili wa Kaa husika ili waone kama kuna Taasisi ina eneo kubwa waweze kuwaombea wanachama hao kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo kama wanavyohitaji.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.