Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe.Hassan Mtenga amewataka Wakuu na Idara na Vitengo Manispaa ya Mtwara-Mikindani kufanya kazi kwa timu na kwa kushirikiana na Ofisi yake ili kuisadia Manispaa katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
‘Tuna kazi ya kufanya kwenye Manispaa yetu, Dira yetu ni Maendeleo, hatuwezi kuwa na maendeleo bila ya kuwa na umoja baina yetu ,tujipange na tufanye kazi kwa kuisaidia Manispaa”amesema Mhe.Mtenga
Ameyasema hayo Agosti 19, 2022 alipozungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Manispaa Agosti 19,2022.
Mtenga amesema kuwa yeye kama Mbunge kazi yake kubwa ni kusaidia upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali hivyo amewataka wakuu wa idara kumshirikisha pale bajeti inapoandaliwa na amewahimiza kusimamia kanuni mara zote wanapotekeleza majukumu yao.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Juliana manyama amemshukuru Mbunge huyo kwa kukutana nao na kumpongeza kwa namna anavyofanya juhudi katika kushughulikia mambo mbalimbali yanayohusu jimbo lake.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.