Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara -Mikindani Mwalimu Hassan Nyange amekabidhi sare 21 kwa Maafisa ugani zilizotolewa na Serikali Kupitia Wizara ya Kilimo ili kuwafanya Maafisa ugani kutambuliwa kiurahisi wanapokwenda kutoa huduma za ugani kwa wakulima na wafugaji.
Mwalimu Nyange amewataka Maafisa hao kuzitunza na kuzitumia vizuri sare walizokabidhiwa kulingana na maagizo yaliyotolewa na Serikali huku akiahidi kuwashonea sare nyingine ili wawe na sare mbili na zisichoke haraka.
Aidha amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii, kuwa na mahusiano mazuri kwenye kazi pamoja na kuwa wabunifu ili waweze kuinua sekta ya kilimo na mifugo na kufilikia lengo la Serikali la kuhakikisha ajenda ya kilimo ya ua 2030 inayosema ukuaji wa sekta ya kilimo ufike 10%.inafikiwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Ushirika, Mipawa Majebele ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuimarisha sekta hiyo muhimu na amemshukuru Mkurugenzi wa Manispaa kwa ahadi aliyoitoa ya kuwashonea sare za ziada na ameahidi kuendelea kuwasimamia kwa ukaribu Maafisa hao kwenye ufanyaji wa kazi zenye tija ili malengo ya Serikali yaweze kufikiwa pamoja na kuwawezesha wakulima kufikia malengo yao.
Zoezi la Ugawaji wa sare kwa Maafisa hhao limefanyika leo Septemba 25, 2024 katika Ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.