Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassani Nyange akiwa ameambatana na watalaam wake leo Octoba 2,2024 amefanya ziara ya kutembelea mradi wa Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari iliyopo Kata ya Tandika, Uwanja mpya wa mpira wa miguu utakaotumika na Shule hiyo pamoja na Zahanati ya Magomeni.
Akiwa katika mradi wa ujenzi Shule ya Sekondari Mpya katika Kata ya Tandika, Mkurugenzi amemuagiza Fundi Mkuu kuongeza nguvu na kasi ya ujenzi huo ili kutimiza malengo na kumaliza kwa wakati uliokusudiwa.
Aidha, ametoa maagizo kwa Mganga Mkuu wa Manispaa (DMO), Elizabeth Oming’o kuhakikisha Zahanati ya Magomeni inakamilisha ujenzi wa kichomea taka (Waste incinerator) ili kufanikisha kutoa huduma ya Wajawazito kujifungua katika zahanati hiyo.
Ziara hii ni ya utangulizi ikiwa Halmashauri inatarajia kupokea ugeni wa Waziri wa Ulinza na Jeshi la kujenga Taifa Mhe. Stergomena Tax anayetarajiwa kuzuru Manispaa ya Mtwara-Mikindani Oktoba 6, 2024.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.