Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani, Mwalimu Hassan Nyange, amewataka walimu kuzingatia maadili ya kazi na kuchapa kazi kwa bidii ili kuzidi kuboresha ufaulu kwa wanafunzi.
Amesema walimu wasibweteke wala kutafuta visingizio bali wachape kazi kwa kutumia rasilimali zilizopo na endapo wataifanya kazi hiyo kwa kujituma basi malengo ya Serikali yatatimia.
Ameyasema hayo wakati wa kufungua mafunzo ya ufafanuzi wa kanuni za maadili ya utendaji kazi katika Utumishi wa walimu ya Halmashauri ya Manispaa Mtwara.
Mafunzo hayo ambayo ni sehemu ya utekelezaji mpango wa Serikali wa mradi wa uboreshaji wa Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) yamefanyika katika ukumbi wa Chama Cha Walimu (CWT) Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Akielezea mikakati ya kuboresha elimu ya Msingi Manispaa ya Mtwara amesema, ataendeleza kushirikiana na walimu wote kutatua changamoto zilizopo na hatamfumbia macho Mwalimu Mkuu yeyote atakayezembea kazini sambamba na kutoa motisha kwa shule zote zitakazofanya vizuri katika ufaulu.
Akizungumzia lengo la mafunzo hayo, Katibu Msaidizi wa Tume ya Utumishi wa walimu (TSC) Wilaya ya Mtwara, Duncan Bushiri, amesema lengo ni kukumbushana kuhusu maadili pamoja na kutoa ufafanuzi wa kanuni za maadili ya utendaji kazi katika utumishi wa walimu.
Amesema maada zitakazojadiliwa ni pamoja Maadili na Miiko ya Walimu, Wajibu wa Mwalimu, Sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma na Ualimu.
@wizara_elimutanzania
@chama_cha_walimu_tanzania
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.