Baada ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kupokea fedha Shilingi bilioni mbili milioni mia mbili ishirini na sita (2,226,000,000) kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika sekta ya afya, elimu, na utawala , Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mwalimu Hassan Nyange amewataka walimu wakuu, wakuu wa shule na watendaji wa Kata ambao wamepokea fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo kuhakikisha wanaanza ujenzi mara moja huku akiwapa siku 60 ya ukamilishaji wa miradi kuanzia Leo Machi 3 ,2024.
Aidha Mkurugenzi amewataka watumishi hao kuwashirikisha wananchi kwenye utekelezaji wa miradi na kuhakikisha wanafanya kazi kwa kushirikiana ili miradi iweze kukamilika kwa wakati kama ilivyopangwa na kwa viwango vilivyowekwa na Serikali .
Mkurugenzi ametoa maagizo hayo Leo Machi 3,2024 alipofanya kikao kazi na watumishi hao kwa ajili ya kuweka mikakati ya ujenzi na ukamilishaji wa miradi hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Miradi itakayotekelzwa na fedha hizo ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi 180,000,000, maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya (1,000,000,000), ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu Shule ya Msingi Rahaleo (128,000,000), ujenzi wa madarasa manne, Ofisi mbili za walimu pamoja na matundu ya vyoo Shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi (126,000,000) na Ujenzi wa madarasa Matano na matundu ya vyoo 8 Sekondari ya wasichana Mtwara (136,000,000).
Miradi mingine ni pamoja na ukarabati wa madarasa ya Shule za Msingi (180,000,000), Ujenzi wa matundu ya vyoo Shule za Msingi 28,000,000, Ununuzi wa Vifaa tiba Zahanati ya Mtawanya (50,000,000) pamoja umaliziaji wa zahanati ya Magomeni (50,000,000) na ununuzi wa vifaa tiba (50,000,000).
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.