Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassani Nyange ametoa rai kwa wazazi kuunga mkono jitihada zinazoanzishwa na shule ikiwamo kushiriki michango ya maboresho ya elimu ili kutokomeza kabisa ufaulu wa daraja la nne na sifuri kwa wanafunzi wa kidato cha nne.
MD Nyange aliyasema hayo wakati akizungumza na wazazi wa wanafunzi wa kidato Cha tatu shule ya Sekondari Mangamba, ili kuweka mikakati mbalimbali ikiwemo kupandisha ufaulu wa wanafunzi hao na kutokomeza daraja la nne na sifuri.
Alisema kuwa wazazi hasa wanaume wanapaswa kuipa kipaumbele elimu ya watoto wao na kuachana na mambo yasio na msingi kama kuwa na wanawake wengi,(michepuko) kwani ni ukweli uliowazi kwamba endapo wataipa elimu kipaumbele hawatashindwa kuchangia michango ya elimu.
Aidha, alitumia hadhara hiyo kuwahakikishia wazazi hao kwamba ifikapo Januari, 2025, hakutakua na uhaba wa walimu ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwani serikali ipo katika mkakati wa kuajiri walimu wapya.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi, Matola Mohamedi, mkazi wa kata ya Tandika-Liyawile, alimpongeza Mkurugenzi kwa kujitoa kwake katika Masuala ya Elimu, huku akieleza shauku yake ya kutaka Mkurugenzi huyo kuwepo Manispaa hiyo kwa muda mrefu zaidi ili aendelee kutatua changamoto mbalimbali za elimu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.