Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya Leo februari 24,2022 amewakabidhi Watoto wenye mahiaji maalumu wanaosoma Shule ya Msingi Rahaleo vifaa mbalimbali vya shule vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Mtwara Economic Development Initiative (MEDI) vyenye thamani ya shilingi milioni moja laki moja na elfu ishirini (1,120,000)
Pamoja na vifaa hivyo Shirika hilo pia limeahidi kutoa usafiri wa kuwapeleka shuleni na kuwarudisha nyumbani wanafunzi hao wanaoishi mbali na shule bila gharama yoyote.
Akizungumza kwa niaba ya Shirika hilo Bi. Clauda Thomasi amesema kuwa shirika la MEDI linamiliki shule binafsi ya awali na Msingi kwa mchepua wa Kingereza na limekuwa na utamaduni wa kuchangia shughuli mbalimbali katika sekta ya elimu, afya na mazingira na kwamba tangu kuanzishwa kwake limeshasaidia walengwa elfu tano mia sita kupata elimu ya Msingi, Sekondari na Ufundi katika Chuo cha VETA.
Afisa elimu Msingi Bi.Flora Aloys amelishukuru Shirika hilo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuendeleza elimu ndani ya Manispaa na kuwagusa watoto wenye mahitaji na kwamba anaendelea kuwakaribisha ili waweze kusaidia Watoto wengi Zaidi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.