Menejimenti ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani wakiwemo wakuu wa Idara na Vitengo Pamoja na wasaidizi wao wakipata chakula cha jioni katika eneo la Bustani ya kupumzikia ya Tilla iliyopo Kata ya Rahaleo.
Chakula hiki kimeandaliwa na Mkurugenzi wa Manispaa Col. Emanuel Mwaigobeko ikiwa ni sehemu ya kupongezana kwa kazi kubwa inayofanywa na watumishi wa Manispaa hii.
Akizungumza katika hafla hiyo Leo April 18,2021 Mkurugenzi wa Manispaa Col. Emanuel Mwaigobeko amewapongeza watumishi kwa kufanya kazi kwa kujituma na kuwataka kutobweteka badala yake kila mmoja kwenye eneo lake ajitahidi kufanya kazi kwa bidi ili Manispaa izidi kusonga mbele.
Amesema kuwa kila mtumishi ana umuhimu wake ndani ya Manispaa na kusistiza watumishi kufanya kazi kwa kushirikiana na kuheshimiana ili Manispaa ifike mbali.
Kwa upande wake Bi. Tamko Mohamedi Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala amesisitiza watumishi kufanya kazi vizuri na pale penye changamoto wasisite kuzitolea taarifa ili zitatuliwe kwa haraka.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.