Baada ya kupokea fedha Shilingi milioni mia sita sitini na sita mia mbili thelathini na tatu (666,233,000) kutoka TAMISEMI za upanuzi wa Zahanati ya Chuno kuwa Kituo cha afya, Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange akiambatana na Wakuu wa Idara na Vitengo Mei 16,2025, wametembelea Zahanati hiyo ili kutambulisha mradi kwa watumishi wa zahanati husika, Watendaji wa Kata, Mitaa na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ya Chuno na Shangani pamoja na kuoneshana eneo linalotarajia kujengwa miundombinu mipya.
Akizungumza katika kikao kifupi na wahusika hao, Mwalimu Nyange amesema kuwa makadirio ya Mhandisi ya ujenzi wa miundombinu mipya katika zahanati hiyo yameshakamilika na kwamba mradi huo unatarajia kuanza mapema mwezi Juni mwaka huu.
Amesema kuwa ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati na kwa ubora, Watendaji wa Kata, Mitaa na Wenyeviti wa Mitaa wanatakiwa kusimamia ujenzi huo kwa kushirikiana huku akiahidi kila mmoja kumpa jengo lake ili alisimamie vizuri.
Wakati huohuo Mwalimu Nyange na timu hiyo walitembelea soko la chuno kuzungumza na wafanyabiashara wachache waliopata vizimba vya biashara ndani ya soko hilo ambao waliwasilisha maombi kwake ya kusamehewa kodi ya pango ya mwaka uliopita ambapo Mkurugenzi ameahidi kuyafanyia kazi maombi hayo na atarudi kuwapa mrejesho.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.