Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe.Shadida Ndile amekutana na wenyeviti wa Mitaa kwa ajili ya kuzungumza nao na Kuwapongeza kwa kusimamia Miradi ya maendeleo iliyotekelezwa Kwenye maeneo yao kuanzia mwaka wa fedha wa 2020/2021 hadi 2024 yenye thamani ya Shilingi bilioni kumi, milioni mia moja sitini na tano, laki tatu thelathini na tatu mia saba hamsini na senti ishirini na moja (10,165,333,750.21).
Mstahiki Meya amewataka wenyeviti hao kuwa wawakilishi wazuri kwa wananchi katika kujibia kero na kutatua changamoto zao kwenye maeneo yao pamoja na kuwa mashuhuda kwa wananchi kwa kuwaeleza mazuri yanayofanywa na Serikali.
Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha zilizosaidia kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu na afya
Pamoja na hayo Mstahiki meya amewataka wataalamu kuendelea kupunguza changamoto ndogondogo huku Serikali ikiendelea kujipanga kukamilisha miradi mikubwa hususani miradi ya maji na barabara.
Ameyasema hayo leo Septemba 18,2024 kwenye kikao na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa CCM Mkoa wa Mtwara ambacho kimehudhuriwa na Taasisi na Idara mbalimbali za Serikali ikiwemo MTUWASA , TARURA, POLISI kilicholenga kuweka mikakati na kukumbushana utekelezaji wa shughuli za maendeleo zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika Kwenye Mitaa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.