Kutokana na baadhi ya wakandarasi kuchelewesha kazi kutokana na kupewa Kazi nyingi za ujenzi wa barabara hapa mjini, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani amewataka TARURA kuepusha kadhia hiyo
kwa kutotoa kazi nyingi kwa mkandarasi mmoja ili kurahisisha utendaji kazi.
Mstahiki ameyasema hayo Leo Agosti 5,2024 alipooongoza kikao cha Kupitia taarifa ya TARURA ya Utekelezaji wa matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2023/2024 na Mpango wa bajeti Kwa miradi ya mwaka Fedha 2024/2025.
Mstahiki Meya amesema kuwa anatambua kazi kubwa inayofanywa TARURA ya ujenzi wa barabara ndani ya Manispaa na ameahidi kuwapa ushirikiano ili kazi za Serikali ziweze kutekelezeka kwa ukamilifu.
Aidha amewataka Madiwani kuwa mabalozi wa kuyasema mazuri yanayofanywa na Serikali kwenye maeneo yao na kutoa Majibu Kwa wananchi pale panapotokea mkanganyiko.
Katika nyakati tofauti waheshimiwa Madiwani waliohudhuria kikao hiko wameipongeza TARURA kwa kazi kubwa wanayoifanya Kwenye maeneo yao ya Utawala na kwamba watafanya kazi Kwa ukaribu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.