Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara -Mikindani Mhe.Shadida Ndile awataka madiwani wa Manispaa hiyo kutoa Elimu kwa vijana kuhusu umuhimu wa mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri kwa vikundi vya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu ili waitumie kama ilivyokusudiwa na kuleta maendeleo katika jamii .
Hayo ameyasema leo, Agosti 1, 2024 katika Mkutano wa baraza la madiwani robo ya nne Kwa ajili ya kujadili taarifa za Halmashauri uliofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa (Boma).
Aidha Mhe.Ndile ameahidi kutatua changamoto zilizopo katika za soko la bomba la bure ili liweze kutumika kwa dhamira ya kuongeza vyanzo vya mapato.
Pamoja na hayo amezitaka kamati mbalimbali za madiwani kushirikiana na watendaji wao bega kwa bega katika kuwahimiza wananchi juu ya umuhimu wa ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuwaweka wazi wananchi katika mikutano ya hadhara kiwango cha mapato kilichokusanywa na matumizi ya mapato hayo katika Utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akielezea kuhusu fedha za mfuko wa Jimbo, Mstahiki Meya amewataka wajumbe wa mfuko huo kusimamia matumizi ya fedha na kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa kweny fedha husika yatekelezwa kwa ushirikishaji na uwazi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.