Kwa mara nyingine tena Mstahiki Meya wa Mnispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Shadida Ndile akiambatana na Madiwani Viti Maalumu Leo februari 26, 2022 amekutana na wanafunzi wasichana wa shule za Sekondari wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa ajili ya kuwapa faraja na kuwatia moyo ili waendelee kusoma kwa bidii na kutimiza malengo yao.
Wanafunzi hao ambao waliambatana na walimu wao walezi wamempongeza Mstahiki Meya kwa kuamua kuzungumza nao na kumuomba semina kama hizo ziwe endelevu na ziwafikie wanafunzi wenge Zaidi.
Aidha Mstahiki Meya amewapatia wanafunzi hao taulo za kike ili waweze kujihifadhi na kuendelea na masomo yao vizuri.
Huu ni muendelezo wa shughuli anazozifanya Mstahiki Meya za kuwatambua mabinti na kuwapa elimu ya Maisha ikiwemo utambuzi wa fursa na kuzichangamkia fursa hizo.
Semina ya kwanza aliifanya Januari 28,2022 katika Ukumbi wa Aflii Mbae ambapo Mstahiki Meya alizungumza na mabinti 150 waliopo mtaani
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.