Kutokana na muitikio mdogo wa wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii , Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Shadida Ndile ametoa rai kwa wanchi wa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani kushirikiana na Serikali katika kutatua Changamoto mbalimbali za Elimu ili kuiunga mkono Serikali katika kuleta Maendeleo.
Amesema kuwa kila mwananchi ana wajibu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za Maendeleo pamoja na kujitoa ili kutatua changamoto zinazoikumba jamii hususani sekta ya elimu.
Mhe. Ndile ametoa rai hiyo Julai 6,2021 katika cha wadau wa Elimu cha Uwasilishaji wa taarifa ya bodi ya mfuko wa Elimu Manispaa ya Mtwara-Mikindani kilichoambatana na Uchaguzi wa Mwenyekiti na wajumbe wapya wa bodi ya Mfuko wa Elimu kilichofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Call and Vision.
"Baada ya Serikali kutangaza elimu bure muitikio umekuwa mkubwa, siis kama wazazi na wadau wa elimu tunawajibu wa kushiriki katika kubotesha elimu nchini, tushirkiane na Serikali katika kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata elimu bora kwa kushirikiana kutatua changamoto katika shule zetu" Alisema Mhe. Ndile
Awali akiwasilisha taarifa ya bodi ya Mfuko wa Elimu Mwenyekiti mstaafu wa bodi hiyo bwana. Smthies Pangisa amesema kuwa kati ya mwaka 2018 hadi 2021 Mfuko huo ulikusanya shilingi 48,933,472 kutoka kwa wadau wa Elimu na katika hizo shilingi 47,478,270 zimetumika kuboresha n akuendleeza ujenzi wa miundombinu katika baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika Manispaa yetu.
Kwa upande wake Mwenyekiti moya wa bodi ya Mfuko wa Elimu Selemani Nahatula ameahidi kushirikiana na wadau wa elimu pamoja n akutoa hamasa kwa wananchi ili kuleta chachu kat9ka kuboresha miundombinu ya ufundishaji katika shule zilizopo ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.