Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe.Shadida Ndile anatarajia kuzindua mashindano ya mpira wa Miguu (Ndile Cup) kwa timu za Kata zote 18, yenye lengo la kuhamasisha wananchi hususani Vijana kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ifikapo Novemba 27, 2024.
Mhe. Ndile amesemwa hayo jana Oktoba 30, 2024 kwenye kikao kilichohusisha waheshimiwa Madiwanj, Maafisa tarafa, Watendaji wa Kata, Viongozi wa timu za mpira za kata, pamoja na wadau wa mbalimbali wa michezo kilichofanyika katika viwanja vya Mashujaa.
Amesema kuwa mashindano hayo yanatarajia kuanza Novemba 9, 2024 katika Viwanja vya Titanic Kata ya Magengeni na fainali itachezwa katika viwanja vya Nangwanda Sijaona ambapo mshindi wa kwanza atapata Shilingi Milioni moja (1,000,000) na mshindi wa pili atapata Shilingi Laki tano (500,000).
Aidha Ndile amewasisitiza Viongozi wa chama na Serikali kuendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura ili waweze kuchagua viongozi ambao watakuwa msingi mkubwa wa kusimamia shughuli za maendeleo
Nae Msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa hiyo Mwalimu Hassan Nyange amesema kuwa licha ya dhana ya kuhamasisha wananchi kupiga kura, wana Mtwara asili yao ni michezo hivyo atafarijika kuona wananchi wengi waliojiandikisha wanapiga kura.
Katika hatua nyingine kupitia kikao hicho Manispaa hiyo imeadhimisha kilele cha maadhimisho ya Siku ya lishe Kitaifa kwa kufanya upimaji wa hali ya lishe, uliohusisha
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.