Watumishi 34 wakiwemo watendaji wa Kata, baadhi ya Wakuu wa Idara ,Maafisa Tarafa na Madereva) wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani wakiongozwa na Mkurugenzi Mwalimu Hassan Nyange pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Shadida Ndile wametua Visiwani Zanzibar kwa ziara ya siku 2 Kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu Uchumi wa buluu (Uchumi unaotokana na shughuli zote za uzalishaji zinazotokana na bahari) na maswala ya Utalii ili Kuongeza mapato Kwenye Halmashauri.
Ziara imeanza Leo Desemba 17,2024 na itamalizika Desemba 18,2024 ambapo Wataalamu hao watatembelea vivutio mbalimbali vya Utalii ikiwemo forodhani, kisiwandui, Kanisa la Mkunazini, Kibwaeni ,Kizimkazi pamoja maeneo mengine.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.