Mfuko wa jimbo uliopo chini ya Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Selemani Mtenga umetoa shilingi 36,513,000 kwa ajili ya kuwezesha ujenzi na ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo iliyopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Mfuko huo ambao upo umeanzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umelenga kuchochea miradi ya maendeleo inayoibuliwa na wananchi.
Miradi iliyopata fedha kupitia mfuko huo ni Pamoja na mradi wa ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Msingi Mjimwema (14,317,500), ujenzi wa matundu ya vyoo vya walimu Shule ya Msingi Magomeni (4,000,000), ukamilishaji wa choo cha mwalo wa Mirumba (3,000,000), ukamilishjai wa choo cha walimu Shule ya Msingi Kwale (2,000,000), Ujenzi wa boma la choo Shule ya Msingi Misufini (2,195,000), kuchangia ujenzi wa Ofisi ya Mtaa Shangani West (1,500,000).
Miardi mingine ni Pamoja na mradi wa uchangiaji wa ujenzi Ofisi ya Mtaa Mjmwema (1,500,000) Pamoja na ununuzi wa siment mifuko 600 kwa ajili ya ujenzi wa miradi mingine ya maendeleo inayotekelzwa ndani ya Manispaa..
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.