Mgogoro uliodumu kwa muda wa miaka kumi kati ya wananchi wa Mangamba( wanaoishi upande wa kaskazini mwa mkuza wa bomba la gesi) na uwanja wa ndefu umefika tamati kwa wananchi hao kurejeshewa maeneo yao na kuruhusiwa kuendelea na shughuli zao za kijamii.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya Septemba 25, 2021 katika kikao chake na wananchi wa Kata ya Mtawanya na Naliendele kilichofanyika katika kiwanja cha Kanisa Katoliki lililopo Shule ya Sekondari ya wasichana Mtwara.
“Eneo la upande wa bomba la gesi kurudi huku limerejeshwa kwa wananchi nina imani na upande ule mwingine tutamaliza mgogoro huu ili tukae kwa amani” Amesema Kyobya
Aidha Mhe. Kyobya ametoa siku 30 kuanza kwa taratibu wa urasimishaji wa maeneo hayo ili kila mwananchi apate eneo na hati ya umiliki kisheria.
Kwa eneo la upande wa Kusini mwa Mkuza wa bomba la gesi ambalo bado lipo kwenye mgogoro Mhe. Kyobya ameahidi kurudi tarehe 15 Octoba kutolea maelezo juu ya maamuzi yaliyofikiwa.
“Tutarudi hapa tarehe 15 Octoba kufanya kikao cha hadhara kuwapa majibu ya mrejesho juu ya upande huo mwingine”Amesema Mhe. Kyobya
Naye Idrisa Sinani Mkazi wa Mangamba ameishukuru Serikali kwa kuwarejeshea eneo hilo na ameiomba Serikali kuendelea kuwapigania ili warejeshewe eneo lililobaki.
Eneo la Kaskazini mwa mkuza wa bomba la gesi (eneo ambalo limerejeshwa) lina ukubwa wa ekari 135 na wananchi wapatao 256 na eneo la upande wa Kusini lenye ukubwa wa ekeri 1250 na wananchi wapatao 1264 .
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.