Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Hassani Mtenga amehaidi ndani ya miaka mitano kujenga barabara za lami kwa kushirikiana na TARURA katika kila Kata ndani ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani ili kuondoa adha zitokanazo na ukosefu wa barabara za rami ikiwemo mafuriko.
“TARURA mnanisikia katika bajeti ijayo tukae mezani tuone tunafanyaje Mwenyezi Mungu akitujalia ndani ya Miaka mitano tunahitaji kila Kata tufungue barabara za rami” Amesema Mtenga
Mhe. Mtenga ametoa ahadi hiyo Oktoba 7, 2021 katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mtonya iliyopo Tarafa ya Mikindani.
Amesema kuwa ukosefu wa barabara za rami katika Kata na Mitaa zinapelekea kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika jamii ziwemo mafuriko na adha ya usafirishaji hasa katika kipindi cha masika.
Ili kutatua changamoto na kuleta maendeleo katika Kata zote zilizopo Mhe. Mtenga amewataka Madiwani na Watendaji wa Serikali za Mitaa kushirikiana kwa pamoja katika utekelezaji wa majukumu yao.
“Rai yangu kwa Watendaji wa Serikali za Mitaa na Madiwani msiwe walalamishi shirikianeni katika majukumu yenu mliopewa” Amesema Mtenga
Amesema kuwa maendeleo ndani ya Kata yanaletwa na ushirikiano baina yao hivyo amewataka kutatua changamoto zilizopo kwa pamoja ili kuleta maendeleo.
Aidha Mhe. Mtenga amewataka Watendaji hao kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa kufanya mikutano ya hadhara ili kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea utatuzi.
Akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Bw. Said Mshamu Kayangu amempongeza Mhe. Mtenga kwa kuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo katika Manispaa yetu na kupigania haki za wananchi wake.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.