Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga 29 Agosti 2021 amezindua mradi wa uchimbaji wa visima 30 katika Kata ya Magomeni Kagera Mtaa wa Kagera ili kurahisisha upatikanaji wa maji kwa kumtua mama ndoo kichwani.
Mradi huo ambao unasimamiwa na Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini utagharimu kiasi cha shilingi Mil 980 hadi kukamilika kwake na utatekelezwa katika vijiji 30 vilivyopo katika majimbo 10 ya Mkoa wa Mtwara, ambapo kila jimbo litapata visima 3.
Ili Mradi huu uwe endelevu Mhe. Mtenga amewataka wananchi wa Mtaa wa Kagera kuhakikisha wanaimarisha ulinzi wa mradi huu kuanzia sasa hadi pale utakapokamilika.
“Visima tunavyovijenga vinahitaji ulinzi wa hali ya juu, mmesikia wenyewe gharama yake ni kubwa mno uangalifu unahitajika sana”Amesema Mhe. Mtenga
Pamoja na hilo Mhe. Mtenga amewataka wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuendelea kujitolea hasa katika Sekta ya Elimu ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha sekta hiyo na kuleta mandeleo.
Naye Mkurugenzi wa Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini Bw. Jumanne Mpemba ameishurukuru Serikali kwa kuwekeza fedha katika mradi huu ambao utapunguza changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo yaliyoanishwa.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Magomeni Bw. Lameck Mlaponi amemshukuru Mhe.Mtenga kwa kuona changamoto ya upatikanaji wa maji katika Kata ya Magomeni na kuitolea ufumbuzi.
Asha Shabani ambae ni mkazi wa Kagera ameishukuru sana Serikali kwa kuwekeza fedha hizo kwasababu mradi huu umepunguza changamoto ya kutumia muda mwingi kutafuta maji.
Kwa Manispaa ya Mtwara-Mikindani visima hivyo viatajengwa katika Kata ya Mitengo, Magomeni na Ufukoni.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.