Mratibu wa huduma ndogo za kifedha Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Janeth Mhegele amevitaka vikundi vinavyojihusisha na huduma ndogo za kifedha (cmg) ndani ya Manispaa kujisajili ili viweze kutambulika na kuweka fedha zao benki badala ya kuweka kwenye masanduku majumbani kama inavyofanyika hivi sasa.
Mhegele ametoa wito huo leo Machi 31,2021 alipokuwa anafanya uhamasishaji kupitia redio juu ya uanzishawaji wa wa sheria mpya ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018 inayotaka vikundi vyote vinavyotoa huduma hiyo kujisajili ili viweze kutambulika rasmi.
Amesema kuwa uanzishwaji wa sheria umelenga kudhibiti na kulinda watumiaji wa huduma ndogo za fedha kuondoa changamoto mbalimbali wanazokutana nazo hizi sasa zikiwemo kuibiwa kwa fedha zinazokusanywa na kutapeliana baina ya wana wana kikundi.
Katika kuhakikisha watoa huduma hao wanazipelkea fedha zao benki kw ajaili ya usalama Mhegele ametoa wito kwa taasisi za kifedha(mabenki) kuhakikisha wanaweka mazingira Rafiki kw avikundi hivyo ili viweze kuweka fedha benki badala majumbani.
Zoezi laUsajili wa huduma ndogo za fedha vikiwemo vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana Pamoja na upatu linaanza rasmi April 1,2021 na litamalizika April 30.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.