Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, amesema kwa kipindi cha miaka minne (2021-2025) ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani, Mkoa wa Mtwara umenufaika kwa kiasi kikubwa kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta zote muhimu.
RC Sawala ameyasema hayo Leo tarehe 04/04/2015, wakati akifungua Kongamano lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Kwa lengo la kujadili Miaka Minne ya Mama Samia Suluhu Hassan, ili kujua 'Tumetoka wapi na Tuko wapi!?', lililofanyika katika Ukumbi wa Songosongo ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) tawi la Mtwara.
"Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma za afya, maji, bandari, barabara, kuboresha uwanja wa ndege, utoaji wa pembejeo za ruzuku, kuboresha miundombinu ya elimu, kuongeza ajira mpya na Kunusuru Kaya Maskini," alisema
Aliongeza kuwa, Miradi hiyo imetekelezwa sambamba na kuimarisha Utawala bora, kutatua kero za wananchi na kuimarisha usimamizi wa miradi ya maendeleo. Uwekezaji huu mkubwa umeboresha utoaji wa huduma za msingi kwa wananchi wa Tanzania na pia kwa nchi jirani za Msumbiji na Visiwa vya Comoro.
Kongamano hilo lilihusisha Viongozi, Wadau wa Maendeleo, na Wananchi wa makundi mbalimbali toka Wilaya zote za Mkoa wa Mtwara ili kujadili mambo mbalimbali yaliyofanyika katika kipindi Cha Miaka Minne ya Rais Samia Madakani, mjadala ulioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdalah Mwaipaya.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilishika hatamu ya kuiongoza Nchi mwezi Machi, 2021.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.