Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Dunstan Kyobya amewagiza watumishi wa Manispaa ya Mtwara-mikindani kufanya mazoezi ya mara kwa mara na kufanya michezo ili kuimarisha na kudumisha mahusiano ya wao kwa wao.
Kauli hiyo ameitoa Ddsemba 8,2022 wakati akifungua bonanza la michezo mbalimbali iliyochezwa na watumishi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya maika 61 ya Uhuru ambapo wameshiriki michezo ya kukimbia na magunia, kunywa soda na mpira wa miguu kati ya watumishi wa Ofisi Kuu na watendaji wa Mitaa .
'Jengeni utamaduni wa kucheza kila mwezi kwa kushirikisha Taasisi mbalimbali ili muondoe vitambi na kuimarisha afya zenu nafikiri inawezekana , michezo pia itaongeza uwajibikaji baina ya watumishi wa Ofisi Kuu na watendaji wa Kata na Mitaa"amesema Mhe.Dunstan Kyobya
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.