Katika kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amewataka wananchi wa Mtwara kuimarisha amani na umoja kwenye kila sekta ili kuimarisha maendeleo ya Taifa letu.
Aidha Mhe. Kyobya amewataka Viongozi wa Kata wakiwemo Madiwani na Wenyeviti wa Mitaa pamoja na kujadili amani kwenye vikao vyao wahakikishe wanahubiri suala la ukatili wa kijinsia Pamoja na mambo mengine hatarishi ambayo kwenye jamii yamekuwa yakifanyika kila siku huku akiitaka jamii kutoa taarifa pale wanapobaini kuna ukiukwaji wa haki za kibinadamu.
“katika kuadhimisha siku hii leo tukataze ukatili wa kijinsia,lakini pia kuna masuala ya ushoga , matumizi ya madawa ya kulevya, wanawake kupigwa vitendo hivi havikubaliki, tusivinyamazie tuwe mashujaa tuseme’ amesisitiza Mhe. Kyobya
Mhe. Kyobya ameyasema hayo leo desemba 9,2022 kwenye kongamano la maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru lililofanyika Chuo Kikuu cha Stella Maris Mtwara likiwahusisha viongozi wa Wilaya ya Mtwara, Madiwani, wazee maarufu, watumishi wa sekta mbalimbali zilizopo Wilaya ya Mtwara Pamoja na wananchi .
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.