Baada ya kufanya kazi kubwa ya kuhamasisha jamii juu ya uchangiaji katika sekta ya elimu na kukusanya fedha kupitia mfuko wa elimu wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Bodi ya mfuko wa Elimu ya Manispaa imefanikiwa kukusanya shilingi 14,978,270 na kuzipeleka katika shule za Msingi na Sekondari kwa ajili ya kukarabati miundombinuya vyoo na madarasa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi kwa shule hizo Julai 1,2020 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya ameipongeza bodi hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuhamasisha na kufanikiwa kukusanya kiasi hiko cha fedha kitakachotumika kukarabati baadhi ya majengo katika Shule.
Pamoja na pongezi hizo Kyobya ameitaka bodi hiyo kuhakikisha inatembelea shule zote zilizopata fedha ili kujua kama zimetumika kama ilivyokusudiwa lakini pia kujua changamoto zilizopo pamoja na mahitaji mengine.
Aidha ametoa siku kumi na sita kwa shule zilizopata fedha kuhakikisha wanakamilisha ukarabati wa miundombinu hiyo na kuwataka walimu wakuu na watendaji wa Kata kuhakikisha kuwa Kampeni ya Shule ni Choo iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa inasimamiwa vizuri.
Awali akisoma taarifa ya Mfuko wa Elimu wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Elimu Bwana. Symthies Pangisa amesema kuwa kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020 Bodi hiyo imekusanya shilingi 14,978,270 kati ya 396,008,000 zilizotarajiwa kukusanywa kutoka kwa jamii.
Amesema kuwa kiasi cha fedha kilichokusanywa kimegawiwa kwa baadhi ya Shule za Msingi za Chuno, Misufini na Sekondari ya SabaSaba na Mitengo kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa matundu ya vyoo Pamoja na kukarabati miundombinu iliyochakaa ya Shule ya Sekondari ya Umoja.
Pangisa amezitaja changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii zilizopelekea kukusanya kiasi kidogo cha fedha ikiwemo uelewa mdogo wa wananchi katika kuchangia Elimu, ugumu wa wnaanchi kuchangia katika elimu Pamoja na uelewa mdogo kwa wasimamizi na wakusanyaji wa michango ya mfuko wa Elimu.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Chuno Bi. Hadija Mkongo ameishukuru bodi kwa fedha hizo na kuahidi kuendelea kuhamasisha na kukusanya fedha za mfuko wa Elimu na kuifanya ajenda ya kudumu kwenye vikao vya Kata.
Mfuko wa Elimu wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani umeundwa chini ya jedwali la kwanza la sharia ndogo ya Uanzishwaji wa bodi ya mfuko wa elimu za halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani za mwaka 2004 katika tangazo la Serikali na 360 la mwaka 2014. Aidha Bodi yaMfuko wa Elimu iliundwa mwishoni mwa mwaka 2017 kwa lengo la kutoa hamasa ya uchangiaji wa mfuko wa kwa jamii,
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.