Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imetumia shilingi milioni ishirini na saba laki nane (27,800,000) kutoka katika mapato yake ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za afua za lishe kwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano kati ya shilingi milioni ishirini na tisa (29,000,000) zilizotengwa katika bajeti ya 2021/2022 sawa na asilimia 92.
Taarifa hiyo imetolewa na Afisa Lishe wa Manispaa bwana Emanuel Moshi kwenye kikao cha maandalizi ya mpango wa bajeti ya lishe ya mwaka 2023/2024 kilichofanyika Novemba 14,2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Aidha kikao hiko pia kimepitisha mpango wa bajeti wa mwaka 2023/2024 ambapo Mnaispaa ya Mtwara-mikindania imekisia kutumia shilingi milioni 71,700,000 kwa ajili ya utekelezaji wa afua za lishe ikiwemo kugharamikia matibabu ya Watoto wenye utapiamolo, ununuzi wa maziwa na virutubishi ,kufanya ukaguzi wa mashamba ya chumvi Pamoja shughli nyingine.
Kikao cha maandalizi ya bajeti kimehusisha wataalamu wa sekta mbalimbali kutoka halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Pamoja na Afisa Lishe kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.