Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani COL. Emanuel Mwaigobeko ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Manispaa fedha shilingi milioni mia nne ishirini (420,000,000) za ujenzi wa madarasa ishirini na moja ya Sekondari ikiwa ni maandalizi ya kujiunga na kidato cha kwanza 2023.
Serikali imetoa fedha hizo ili kuhakikisha kuwa miundombinu katika sekta ya elimu hapa nchini inaboreshwa na kuwekewa mazingira wezeshi ya kufundishia na kujifunzia katika shule zilizopo Mnaispaa ya Mtwara- Mikindani.
Ujenzi wa madarasa hayo ukishakamilika unaenda kuondoa kabisa tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa upande wa elimu Sekondari na hivyo Manispaa inatarajia kuweka mazingira wezeshi kwenye ufundishaji ili kuongeza kasi ya ufaulu kwa wanafunzi.
Shule zilizopokea fedha hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Chuno ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa (40,000,000), Shule ya Sekondari ya Mangamba vyumba viwili vya madarasa (40,000,000), Shule ya Sekondari ya Saba Saba vyumba viwili vya madarasa (40,000,000), Shule ya Sekondari Mitengo ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa (40,000,000).
Shule zingine ni Pamoja na Shule ya Sekondari ya Mikindani ujenzi wa chumba kimoja cha darasa (20,000,000), Shule ya Sekondari ya Naliendele ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa (60,000,000), Shule ya Sekondari ya Shangani ujenzi wa vyumba vitatu vya madarsa (60,000,000), Shule ya Sekondari ya Sino Tanzania Friend Ship madarasa Matano (100,000,000) Pamoja na Shule ya Sekondari Umoja wa darasa moja (20,000,000).
Madarasa haya yakishakamilika yataondoa changamoto wa uhaba wa madarasa kwneye Shule zote za Sekondari.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.