Ili kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi katika bustani yetu ya kupumzikia ya Mashujaa na eneo la bustani ya mbogamboga Indian quartes, kupitia mapato yetu ya ndani tumeanza uchimbaji wa visma virefu viwili vya maji vyenye urefu wa jumla ya Mita 150 kwa gharama ya shilingi 42,750,000
Tayari zoezi la uchimbaji wa kisma kirefu cha maji chenye urefu wa Mita 80 limeanza eneo la Mashujaa kama inavyooneka kwenye picha na baadae zoezi hili la uchimbaji wa kisima cha maji chenye urefu wa Mita 70 litaendelea katika eneo la bustani ya mbogamboga inayoendeshwa na wajisiriamali wadogo wadogo iliyopo Indian Quartes.
Visima vyote vitachimbwa kwa siku kumi kupitia makandarasi kutoka Kampuni ya A’S Technologies iliyopo Mtwara.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.