Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange kupitia mfuko wa elimu ameahidi kutoa fedha Shilingi milioni arobaini na tatu laki tano tisini ( 43,590,000) kwa shule 11 za Serikali za Kutwa kwa ajili ya mahitaji ya kambi kwa wanafunzi wa kidato cha nne.
Mkurugenzi anatoa fedha hizo ikiwa ni mkakati mmoja wapo wa kuweka mazingira mazuri ya kujisomea kwa wanafunzi na kujiandaa vema kwenye mtihani wao wa kumaliza Elimu ya Sekondari ili Kuongeza ufaulu na kufuta daraja sifuri.
Hayo yamesemwa Leo Januari 27,2025 katika Kongamano la elimu lililofanyika katika viwanja vya Mashujaa, lenye lengo la kuhamasisha ufaulu na kuweka mikakati ya kuondoa daraja sifuri.
Amewataka Wakuu wa Shule kukaa na wazazi kuwahimiza michango ya kambi na kupongeza kuwa, Halmashauri inaendelea kupambana kuhakikisha kambi inaleta tija.
Vile vile amewaasa wanafunzi wa kidato cha nne kutopoteza muda kwa kuangalia tamthilia zisizo na maana badala yake wasome vitabu mbalimbali vitakavyo wasaidia kuongeza maarifa
Shule zitakazohusishwa na mgao huo ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Shangani,Rahaleo,Mangamba,Sino Tanzania Friendship,Sabasaba,na Naliendele.
Shule nyingine ni Shule ya Sekondari ya Umoja,Bandari,Mikindani,Chuno na Mitengo Sekondari.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.