Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange amesema kuwa jumla ya miradi sita yenye thamani ya Shilingi milioni mia tisa tisini na tano mia tano kumi na moja mia nne na nne (995,511,404) itatembelewa na Mwenge wa Uhuru leo Mei 25,2025.
Amesema kuwa kati ya miradi hiyo, miradi minne itazinduliwa ( mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Msikitini- Majengo, mradi wa ujenzi wa kisima cha maji Mtaa wa Mwera- Chikongola), Shule ya Sekondari ya Tandika na uzinduzi wa jengo la redio la HFM),
Mradi mmoja utawekwa jiwe la Msingi(Ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje zahanati ya Mtawanya) pamoja na kuona na kukagua mradi wa vijana wa ujenzi na uzalishaji wa malighafi ya ujenzi Uliopo Mtaa wa Mbae Mashariki katika Kata ya Ufukoni.
Mwalimu Nyange ameyasema hayo wakati akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Abeid Kafunda katika eneo la soko la Mirumba -Mikindani.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.