Mratibu wa Mwenge Manispaa ya Mtwara-mikindani Nicholous Semwene amesema kuwa miradi sita kutoka katika seta ya elimu, afya, barabara na maji yenye thamani ya shilingi bilioni mbili milioni mia nane themanini na nane mia nne kumi na moja (2,888,411,000) inatarajiwa kutembelewa na mwenge wa Uhuru April 2, 2023.
Semwene ameyasema jayo Janurai 9,2023 kwenye kikao cha wadau wa maendeleo kilichoitishwa na Mhe .Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya ambapo viongozi mbalimbali na wataalamu kutoka halamshauri tatu za Wilaya ya Mtwara walihudhuria kujadili mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ambapo Kitaifa utawashwa Mkoani Mtwara April 2, mwaka huu.
Katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya alisisitiza uundaji wa kamati mbalimbali za hamasa kuanzia kwa Wenyeviti wa Mitaa hadi kwa Viongozi wa dini..
Mhe .Mkuu wa Wilaya pia alitoa taarifa ya uwepo wa amshindano ya michezo ya majeshi (BAMMATA) itakayoanza februari 9 hadi februari 21 mwaka huu ambapo washiriki 1200 watakuwepo
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.