Badala ya wakulima kutegemea ulimaji wa zao moja la korosho,Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Hanafi Msabaha amewataka wataalamu wa Halmashauri zilizopo Wilaya ya Mtwara kuhakikisha wanawahamasisha wakulima wilayani hapa kulima zao zaidi ya moja ili wasitetereke inapotokea changamoto kwenye uzalishaji wa zao hilo.
Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo Februari 13’2023 alipokuwa anafungua kikao cha Kamati ya Ushauri cha Wilaya kilichofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Call Vision.
Aidha Mhe. Mkuu wa Wilaya amewataka wataalamu hao kuhakikisha wanaimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi pamoja na usimamiaji mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye halmashauri zao ili ubora wa majengo na thamani ya pesa ionekane .
Ili kuimarisha utawala bora Msabaha amewasisitiza wataalamu kujenga tabia ya Kuwatembelea wananchi ili kufahamu changamoto zinazowakabili na kutafuta njia nzuri ya kuzitatua changamoto hizo.
Kwa upande mwingine Msabaha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta za afya, elimu Pamoja na sekta zingine.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.