Hayo yamezungumzwa jana Mei 8 na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani bi Beatrice Dominic wakati akifungua mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini ya Miradi kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya kata Vigaeni.
Beatrice amesema kuwa Afisa Maendeleo ya jamii anayeijua kazi yake anatakiwa kuwa chanzo cha Maendeleo kwa jamii anayoihudumia kwa kuwasaidia wana jamii hao kuwa wabunifu kwenye uibuaji wa miradi yenye tija itakayoleta manufaa kwao. Ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo itavutia hata sekta nyingine kama mabenki na makanisa kuwatumia kwenye shughuli za uwezeshaji.
Aidha Baetrice amewataka Maafisa hao kutoa ushirikiano mzuri kwa jamii na kufuatilia miradi inayotekelezwa ili iweze kukamilika kwa wakati.
‘’kumekuwepo na ushirikiano mdogo kati yenu na jamii inayozunguka miradi, jamii ingehamasishwa kuhusu miradi nina imani wana jamii wangesaidia kubeba zege, kuchimba msingi,kubeba mawe na kupelekea kupunguza gharama za mradi huo, shirikisheni jamii ili miradi ikamilike kwa wakati ”. Alisema Beatrice
Kwa upande wake muwezeshaji wa mafunzo hayo Bi Tabitha Kirangi amewasisitiza maafisa hao kutumia taaluma zao katika kupanga miradi inayopaswa kutekelezwa kwa kuangalia fursa zilizopo kwenye eneo husika.,ameongeza kuwa kinyume na hapo unaweza kutekeleza mradi ukaleta hasara kwa jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mendeleo ya jamii bi Juliana Manyama amesema kuwa mafunzo hayo ni ya kwaida yakiwa nalengo la kukumbushana majukumu katika utendaji wa kazi na kwama wao kama kitengo wamejipanga kufanya kazi kwa kufuata maadili,kanuni na miongozo mbalimbali iliyowekwa ili kuisaidia jamii.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.