Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani, Mwalimu Hassan Nyange ameipongeza Shule ya Sekondari Mtwara Ufundi kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne na kuwataka wanafunzi watakaomaliza awamu ijayo kufanya vizuri zaidi.
MD Nyange ameyasema hayo wakati akiongea na wanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo, ikiwa ni utaratibu wake wa kawaida kuzungumza na wanafunzi na kuwatia moyo lakini pia kuipongeza shule hiyo kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni.
Alisema hakuna kinachoshindikana katika Dunia, hivyo akawataka wanafunzi hao kutia nia, kuweka bidii na kuwasikiliza walimu ili wafaulu mitihani yao na kufanikiwa katika maisha.
Aliongeza kuwa changamoto za umasikini na hata hali ya ulemavu inapaswa kuwa chachu ya wao kufanya vizuri na si kisingizio cha kushindwa.
"Lazima ujue unataka uwe nani katika maisha, ukikaa hapa iuvute taswira ya familia yako kichwani, wakumbuke wazazi wako... na utambue kwamba inaweza kuwa mkombozi wao," alisisitiza.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.