Mkoa wa Mtwara umeongoza Kitaifa katika zoezi la utoaji wa chanjo ya UVIKO-9 kwa kuchanjwa watu wapatao 17631 sawa na asilimia 83%
Zoezi hilo ambalo lilizinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig.Marco Gaguti Agosti 3, 2021 na kupelekea Mkoa wa Mtwara kuvuka lengo la kimkakati na kuchanja watu wapatao 17631 hadi kufikia Septemba 30,2021.
Taarifa hiyo imetolewa Septemba 30, 2021 na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya katika Kikao cha Kamati ya ushauri ya Afya ya Msingi Wilayani kilichofanyika katika Ukumbi wa Polisi Mess Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
“Kitaifa tumeongoza, niwapongeze wataalamu na wadau wote waliofanya hamasa na kutoa elimu, kwa juhudi zao tumeweza kupeleka ujumbe na wananchi wakahamasika na kuchanja” Amesema Mhe. Kyobya
Aidha Mhe. Kyobya amesema kuwa kamati hiyo bado ina kazi kubwa ya kuendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi ili jamii itambue umuhimu wa chanjo hiyo na kuamua kuchanja kwa hiyari.
”Kimkakati ytumevuka leongo ila kwa idadi ya watu bado hatujafikia lengo ila kwa idadi ya watu bado hatujafikia lengo kazi ya kamati hii ni kutoa elimu na hamasa ili kila mwananchi atambue umuhimu na kuchanja” MAmesema Mhe. Kyobya
Naye Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Hassani Mtenga amewataka wananchi kuendelea kupuuza taarifa za upotoshaji dhidi ya chanjo ya UVIKO-9 na kuungana na Serikalai katika kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa UVIKO -19
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.