MKURUGENZI KUTUMIA MAPATO YA NDANI KATIKA KUTOA ELIMU YA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO.
Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara-Mikindani bi Beatrice Dominic ameahidi kutumia sehemu ya fedha kutoka katika makusanyo ya mapato ya ndani katika kutoa elimu kwa baadhi ya Kata ambazo hazijashiriki katika mafunzo ya ushughulikiaji wa malalamiko.
Amesema kuwa Elimu hiyo itatolewa na washiriki waliopata mafunzo hayo kwa watumishi wengine ili kujenga uelewa kwa watumishi katika kushugulika malalamiko yanayofika katika Ofisi zao.
Bi Beatrice alizungumza hayo siku ya septemba 26, 2017 kwenye mafunzo ya namna ya kushughulikia malalamiko yanachofanyika kwenye hoteli ya Tifany iliyopo Manispaa Mtwara-Mikindani.
Pia amewataka Maafisa malalamiko kuwa makini katika utoaji wa taarifa kwa wakati kwani kwa kufanya hivyo kutajenga imani kwa wateja na itapelekea kasi ya malalamiko kupungua. Aidha amewataka Maafisa malalamiko hao kupeleka kwake malalamiko yote ambayo watashindwa kuyatatua.
Vilevile amewasisitiza Maafisa hao kuthamini kila mtu anayefika kwenye Ofisi zao na kutumia ujuzi walioupata kwenye mafunzo katika utendaji wao wa kazi wa kila siku, na amewataka kutambua kuwa sio kila lalamiko lina ukweli na kwamba wao kama viongozi wanaweza kusingiziwa uongo wasikate tama a na wanatakiwa kuwa wavumilivu.
Pamoja na hayo Bi Beatrice amesisitiza kuwa kila mtumishi wa umma kwa nafasi yake anatakiwa kutekeleza wajibu wake ili kupunguza malalamiko labda kwa yale yaliyopo nje ya uwezo wa halmashauri kama ujenzi wa barabara na sehemu zingine.
“Ninawaambia kama kila mtu kwa nafasi yake atatekeleza wajibu wake tutapunguza malalamiko,kashughulikieni malalamiko” alisema Beatrice.
Ameongeza kuwa faida kubwa ya kushughulikia malalamiko kwa wakati ni pamoja na kuboresha utendaji wako wa kazi pamoja na kujenga mahusiano mazuri kati ya Serikali na Wananchi, Taasisi ambayo haishughulikii malalamiko Wananchi wake wanakata Tamaa.
Aidha amewaahidi Waheshimiwa Madiwani waliopo kwenye mafunzo hayo kuwa kwenye kikao kijacho cha baraza la madiwani la kujadili taarifa za kwenye Kata atawapa muda wa dakika thelathini ili waweze kutoa mafunzo kwa Madiwani wasiopata mafunzo,hii pia itawahusu walimu na watendaji.
Mafunzo ya malalmiko yamefadhiliwa na Shirika la uimarishaji wa mifumo wa sekta a umma(PS3) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Kwa Tanzania halmashauri ya Bahi,Kishapu,Kigoma Ujiji pamoja na Manispaa Mtwara-Mikindani ni halmashauri peee zilizoteuliwa kwenye uppataji wa mafunzo yahusuyo ushughuliakiaji wa malamiko.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.