Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange amekutana na Wakuu wa Idara na Vitengo, Maafisa tarafa pamoja na Maafisa watendaji wa Kata na Mitaa na kuweka mikakati Madhubuti ya kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake katika kuweka Mji wa Mtwara safi wakati wote.
Mwalimu Nyange amesema ili kuweza kutimiza adhma hiyo Manispaa itanunua maguta .yenye thamani ya Shilingi milioni sabini (70,000,000) katika bajeti yam waka ujao ambayo yatakuwa yanakusanya takataka kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi kama vile masokoni na magari ya kubeba taka yaliyopo yatakuwa na kazi ya kuzoa takataka kutoka kwenye vizimba na kupeleka dampo kuu.
Aidha amewasisitiza Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kufanya kazi kwa kushirikiana na kuhakikisha wanafanya hamasa kwa wananchi ya kuwataka kusafisha maeneo yao kuwasimamia na kutoza faini kwa wale wote watakaokaidi kufanya usafi ili kila mmoja awajibike.
Wakati huohuo Mkurugenzi amewataka Maafisa hao kujiandaa vema kwa kufanya hamasa ya kutosha kwenye maeneo yao kwa kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru unaotarajia kuwasili Manispaa ifikapo Mei, 25,2025
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.