MKUU WA MKOA WA MTWARA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI NA WAZEE MAARUFU MJINI MTWARA.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius E. Byakanwa Novemba 21, 2017 amefanya kikao cha pamoja na wazee maarufu pamoja na Viongozi wa dini Wa Mtwara Mjini kwa lengo la kujitambulisha na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Mkoa.
Katika kikao hiko ambacho kilifanyika katika ukumbi wa Boma Mkoa Mkuu wa Mkoa alizungumza mambo mengi yanayowahusu wazee pamoja na wana Mtwara kwa ujumla. Aidha Mkuu huyo alisema kuwa amefurahishwa wazee na viongozi hao kuitikia wito wake na kwamba imemuonesha kuwa wenyeji wapo na amepokelewa vema.
Mheshimiwa Byakanwa alisema kuwa kutokana na umri waliokuwa nao wazee hao ni lazima mabenki yatenge dirisha maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wazee hao, akina mama wajawazito pamoja na watu wenye mahitaji maalumu.
Aidha kwa upande wa zao la korosho amesema kuwa Serikali ya Mkoa imeagiza malipo ya wakulima yote yapitie benki na kwamba wakulima wahamasishwe kufungua akaunti kwa ajili ya kutunza fedha zao. Ameongeza kwa kuwataka wakulima hao kuwa na utamaduni wa kuweka akiba na kwamba wanapoenda kutoa fedha benki watoe kidogo kidogo kwakuwa kukaa na fedha nyingi nyumbani inahatarisha usalama wa maisha yao.
Pia amewataka wafanyabiashara wa korosho wote kutumia bandari ya Mtwara kusafirisha korosho zao kwa kuwa serikali kuu ilishatoa fedha kiasi cha shilingi bilioni …… kwa ajili ya upanuzi wa bandari hiyo. Hata hivyo amesema hadi wiki iliyopita Bandari ilishakusanya shilingi bilioni 24 tangu msimu ulipoanza.
Kwa upande wa Elimu Mkuu wa Mkoa amesema haridhiki na matokeo ya mtihaniwa taifa wa darasa la saba ambapo Mkoa upo kwenye nafasi tano za mwisho na hivyo amemuagiza Katibu Tawala tawala aitishe kikao cha wadau wa Elimu ili waweze kujadili changamoto za elimu na namna ya kuzitatua.
Byakanwa amewataka Wakurugenzi kuhakkisha kuwa wanachi wao wamekata bima ya afya nakwamba baada ya msimu kumalizika aandaliwe taarifa itakayoonesha wanachi walojiunga kwenye mfuko wa bima ya afya.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.