Mkuu Wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Danstan Kyobya amempongeza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Ufundi Mtwara kwa kutumia ubunifu wa kuwashirikisha wanafunzi wa shule hiyo katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 2 vinavyojengwa shuleni hapo kupitia Mpango wa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.
“Nikupongeze huu ni ubunifu mkubwa umeonesha, hawajifunzi tu kwa vitendo lakini wamepata somo la kuwa wazalendo” Amesema Kyobya
Mhe . Kyobya ametoa pongezi hizo Novemba 4,2021 katika Ziara ya Kamati Kuu ya Mkoa wa Mtwara ilipotembelea kukagua na kupokea taarifa ya utekelezaji wa madarasa yanaoyojengwa kupitia Mpango wa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Amesema kuwa ubunifu huo ni funzo kubwa la ushirikishwaji wa wananchi na kusisitiza kuwa ushirikishwaji wa wanafunzi hao hautaathiri ubora wa madarasa hayo kwa kuwa kuna wataalam wanaosimamia ujenzi huo.
Ili kukamilisha madarasa hayo kwa wakati na kwa ubora unaohitajika Mhe. Kyobya amemtaka Diwani wa Kata ya Shangani Mhe. Abuu Mohamedi kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi wa Kata hiyo ili kushiriki katika ujenzi huo.
Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Shangani Mhe. Abuu Mohamed amemhakikishia Mhe. Kyobya kumaliza ujenzi wa madarasa hayo ndani ya Muda uliopangwa na katika ubora zaidi.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bandari Bi. Amina Bakari amewashukuru wananchi wa Kata ya Reli kwa ushiriki wao na amewataka kujitokeza zaidi katika hatua zinazofata.
Naye Asha Jumanne Mwanafunzi wa Kidato cha Pili katika Shule ya Ufundi Mtwara amemshukuru Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa kupunguza changamoto ya madarasa katika Shule yao.
Kamati hiyo imetembelea Ujenzi wa vyumba vya madarasa Sekondari ya Sabasaba,Bandari, Shangani,Chuno,Magomeni ,Mitengo Mangamba na Naliendele pamoja na Shule ya Msingi Mitengo na Kamabarage,
Pia imetembelea Ujenzi wa nyumba ya Mganga Zahanati ya Rwelu na Ujenzi wa Jengo la kujifungulia Zahanati ya Ufukoni pamoja na Upandaji miti iyopo chini ya mradi wa Kaya Maskini TASAF.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.