MPANGO KABAMBE UMEKUJA KUONGEZA THAMANI YA ARDHI.
Wananchi wa Mtwara wametakiwa kutokuwa na hofu na uwepo wa Mpango kabambe wa Mji wa Mtwara kwani uwepo wake utasaidia kuinua thamani ya ardhi ya Mtwara kwa kuwa ardhi hiyo imepangika vizuri.
Hayo yamesemwa jana na Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. William Lukuvi wakati wa uzinduzi wa Mpango kabambe wa Mji wa Mtwara uliofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara .
Waziri Lukuvi alisema kuwa uwepo wa mpango huo utasaidia Mji kupangika vizuri na hivyo kuvutia wawekezezaji kuja kuwekeza Mtwara kwa ajili ya ujenzi wa viwanda mbalimbali. Aidha alisema kuwa Serikali imejipanga kuleta wawekezaji wengi Mkoani Mtwara.
Mh Lukuvi aliendelea kusema kuwa Mpango huo haukuja kunyang’anya ardhi ya mtu wala kubadilisha mipaka ya kiutawala iliyopo kati ya halmashauri mbili ambazo zimeunda mpango kabambe huo. Badala yake uendelezwaji wa maeneo ya mpango yatafanywa pamoja na kila Halmashauri itapata mapato yake.
Aidha amewataka Waheshimiwa Madiwani na Watendaji wa Idara ya Ardhi kuacha kudai rushwa ili waweze kupitisha maombi ya ramani za ujenzi.
“Waheshimiwa Madiwani na Watendaji acheni kupokea rushwa iili wananchi wapitishiwe ramani zao mnachelewesha Maendeleo”alisema Lukuvi.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Mtwara aliishukuru Wizara kwa kusimamia jambo hili na hatimae limezinduliwa rasmi, aidha alisema kuwa uwepo wa mpango huo utasiaidia kutatua migogoro mingi ya ardhiambayo ni changamoto kubwa kwenye halmashauri zetu.
Awali akisoma taarifa ya Mpango Kabambe wa Mji wa Mtwara Afisa MipangoMiji wa Manispaa Mtwara Mikindani Hamza Sikamkono alisema kuwa Mchakato huo ulianza mudamrefu na kwamba sababu zilizopelekea uwepo wa Mpango kabambe ni pamoja na Ongezeko la idadi ya watu,ongezeko la mji,ugunduzi wa miradi ya gesi, mpango wa Taifa wa kuiendeleza Mtwara.
Nae Afis ardhi wa halmashauri ya Wilaya ya Mtwara alibainisha maeeno matano ya mpango ikiwemo…………
Mpango kabambe wa Mji wa Mtwara unahusisha halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani pamoja na halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Mpango huo unahusisha kata 18 zilizopo Manispaa na kata 9 kutoka halmashauri ya wilaya ya Mtwara.Mpango huu utadumu kwa miaka 20 kuanzia 2015-2035.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.