Makarani wa Sensa, wasimamizi wa maudhui ya sensa na Wataalamu wa TEHAMA wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Kaspar Mmuya alipowatembelea kwenye mafunzo Agosti 16,2022
Naibu Katibu Mkuu Ofisi yaWaziri Mkuu Bunge ,sera na uratibu bwana Kaspar Mmuya amewataka makarani wa sensa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kutoongeza idadi ya watu kwenye zoezi la uingizaji wa taarifa za sensa ya watu na makazi badala yake watoe taarifa zenye uhalisia zitakazoisaidia Serikali katika kupanga mipango ya Maendeleo ya Taifa.
Naibu Katibu Mkuu ameyasema hayo Agosti 16,2022 alipowatembelea makarani wa sensa kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo Cha Stella Maris Kilichopo Mtwara.
Bwana MMuya amewasisitiza makarani hao kujiandaa vizuri kwa kuwa na takwimu za awali za Msingi kwenye eneo analoenda kufanya kazi ikiwemo idadi ya kaya ya eneo hilo ili kurahisisha zoezi hilo..
Aidha amewataka kuwa makini juu ya matumizi ya vishkwambi kwa sababu ni mali ya serikali na wanatakiwa kuvizoea kuvitumia vifaa hivyo mapema ili wanapoenda eneo la kazi isiwe na vikwazo kwenye kuvitumia.
Ameendelea kuwasisitiza makarani hao kuendelea kutoa hamasa ili watu wajitokeze kuhesabiwa Pamoja na kutoa taarifa mapema itakapotokea dosari wakati wa zoezi ili waweze kupata msaada wa haraka .
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.