Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange amewahamasisha wananchi wote wenye umri unaoanzia kuanzia miaka kumi na nane(18) na kuendelea kushiriki kikamilifu kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwemo Kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura katika vituo vitakavyotangazwa hapo baadae.
Amesema kuwa zoezi la Uandikishaji litaanza rasmi Oktoba 11 na litakamilika Oktoba 20,2024
Aidha Mwalimu Nyange amesema kuwa Manispaa imeandaa bonanza la mchezo wa mpira wa miguu la watumishi kati ya watumishi ambao ni mashabiki wa timu za Simba na Yanga ili kuleta hamasa na Umoja kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Amebainisha kuwa bonanza hilo litafanyika siku ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa Oktoba 14, 2024 (Nyerere Day) katika Viwanja vya Nangwanda Sijaona.
Mwalimu Nyange ameyasema hayo Septemba 29, 2024 kwenye fainali ya tamasha la Michezo la Mtonya ( MTONYA FESTIVAL) lililofanyika katika viwanja vya ghala la kuhifadhia Korosho katika Kata hiyo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.