Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Shadida Ndile akiambatana na waheshimiwa madiwani wengine leo novemba 10,2022 amekutana na wanafunzi wanaosoma Chuo Cha VETA Mtwara ambao ni raia wa COMORO na kupata nao chakula cha mchana lengo ikiwa ni kufahamiana nao na kuwatia moyo kwenye masomo yao.
Aidha kutokana na kutofautiana kwa baadhi ya mambo fulani kati ya nchi ya Comoro na Tanzania Mstahiki Meya amewahimiza wanafunzi hao kuwa na uvumilivu na kuendelea kujifunza taratibu ili waweze kutimiza malengo yao.
“Ninafahamu kule kwenu chakula aina ya ugali hakuna, lakini hapa mmekutana nacho na mtaendelea kukutana nacho tujitahidi kujifunza taratibu mtazoea na mambo yatakuwa rahisi”amesisitiza Mstahiki Meya.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mtwara Mjini ndugu amewakaribisha wanafunzi hao Manispaa ya Mtwara-Mikindani huku kuwaahidi kuzidi kuwalinda na kuwataka kuweka nguvu kwenye kujifunza ili wakirudi nyumbani wawe wameiva. Aidha amewataka kutoa taarifa kwenye ofisi za Chama pale wanapopata matatizo.
Kwa upande wake msaidizi wa Gavana wa Ndzuwani Comoro Bwana Abdou El Anziz Said Attoumani amesema kuwa wanafunzi hao wamekuja Tanzania kusoma masomo ya Ufundi ili wakirudi Comoro waweze kujiajiri na kuwaomba Madiwani kuwapokea na kuwalea wanafunzi hao kwa kuwa hapa Mtwara hawana ndugu yeyote.
Wanafunzi 11 kutoka COMORO wamefika nchini Tanzania Novemba 9,2022 wakipokelewa na Viongozi mbalimbali wa Mtwara akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya, Mstahiki Meya wa Mnaispaa ya Mtwara-mMkindani Mhe. Shadida Ndile Pamoja na viongozi wengine.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.